OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RC-Kitwana atoa pole kwa waathirika wa moto Kiponda, Mjini Zanzibar
HabariHabari Mpya

RC-Kitwana atoa pole kwa waathirika wa moto Kiponda, Mjini Zanzibar

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amewataka Wakaazi  wa Mji Mkongwe  kuchukua tahadhari dhidi ya miripuko ya moto amesema hayo wakati alipotembelea  kwenye eneo la tukio la kuungua moto nyumba katika Sheha ya Kiponda  Mkoa wa Mjini Magharibi na kutoa pole kwa familia zilizo athirika .

Aidha ametoa pole kwa familia ya marehemu Bi Rehema Chande Chande ambae alifariki alipokuwa akijihami akiwa amembeba mjukuu wake Nabili Issa Ramadhani mwenye umri wa miaka 5, ambae yupo hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kwa matibabu zaidi.

Nae shuhuda  wa tukio hilo Bw. Seif  Omar Hamad amesema Chanzo cha moto huo ni hitilafu  za vifaa vya umeme katika  Nyumba ya marehemu na kupelekea kuvunja Nyumba hali iyopelekea kujitupa kutoka juu hadi chini kwa kuokaa maisha ya mjukuu wake  na kupelekea kifo chake  aidha amesema chanzo hicho kutokana  na kukosekana kwa msaada wa haraka.

 Nae Sheha wa Shehia hiyo ambae pia Muathirika  wa  tukio hilo Mh.Juna Khamis Makame amesema marehemu Bi Rehema Chande Chande  amepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 71. Marehemu alikuwa anakaa Nyumba nambari 1508 Kiponda zaidi ya vyumba 7 vimeathirika na moto  na hakuna thamani wala kifaa chochote kilichopatikakana, Pia nyumba ya jirani nambari 1509  yenye familia 3 imeathirika. 

Katika eneo hilo la tukio limehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya, Mstahiki Meya, Katibu Tawala Mkoa na Wilaya ya Mjini, Kamishina wa Zimamoto, Maafisa wa Polisi, Madiwani, Masheha na Wananchi.