OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RC apokea vifaa Tiba na Dawa kwa ajili ya Hospital ya Mpendae
HabariHabari Mpya

RC apokea vifaa Tiba na Dawa kwa ajili ya Hospital ya Mpendae

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amelishukuru  Jeshi la Wananchi Tanzania na Jeshi la Uganda wakati wa upokeaji wa msaada wa dawa na vifaa tiba katika Kituo cha afya Mpendae.

Amesema Jeshi la Wananchi Tanzania linafuata dhana ya Baba wa Taifa kuwa karibu na Wananchi, pia ameasema dawa na vifaa tiba hivyo viwe  chachu kwa maendeleo ya Wananchi.

Aidha Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi amepokea msaada huo kwa Bregedia Jenerali Emmanuel Rwashande kutoka Jeshi la Uganda na Bregedia Jenerali Said Khamis kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania Utoaji huo wa dawa na vifaa tiba ni shamra shamra ya kuadhimimisha siku ya Majeshi ya Afrika Mashariki na Kati.

Nae Bregedia Jenerali Emmanuel Rwashande amesema msaada huu umelenga  kuadhimisha siku ya Wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  na kuambatana  Madaktari bingwa wa Jeshi la Uganda ili kuweka karibu Wanachama wa Jumuiya hiyo.

Aidha Bregedia Jenerali Said Khamis amesema maadhimisho haya yatagusa zaidi maeneo ya huduma za watoto na watu wazima.

Maadhimisho ya wiki ya Jeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianza kuazimishwa mapema nchini Uganda mwaka 2018 na 2019 na mwaka 2020 imekosekana  kwa sababu ya janga la UVIKO 19, mwaka 2021 iliadhimishwa nchini Kenya na kwa mwaka huu 2022 inafanyika nchini Tanzania.

Maadhimisho  hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Katibu Tawala  Mkoa wa Mjini Magharibi , Katibu Tawala  Wilaya ya Mjini , Masheha na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi.