OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Karibu Mkoa wa Mjini Magharibi

Video

Mhe. Idrissa K. Mustafa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi , inayo furaha kukukaribisha katika tovuti hii. Tunatumaini utapata taarifa zetu mbali mbali, huduma, makala na mengi mengineyo yanayohusu shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ndani ya Mkoa Mjini Magharibi. Ni matumaini yangu kuwa kila atakayetembelea tovuti hii atahabarika, ataelimika na atafurahika. Tunafurahi sana kupata maoni na ushauri wa watembeleaji wa tovuti hii na tunathamini  kila maoni tutakayoyapokea.

Historia ya Mkoa Mjini Magharibi

Kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964 Zanzibar iligaiwa jiografia katika maeneo makubwa matatu yaliyopewa hadhi ya Wilaya ambayo ni :-

  • Wilaya ya Mjini
  • Wilaya ya Mashamba
  • Na Wilaya ya Pemba

Kutokana na hali hiyo Zanzibar baada ya Mapinduzi ikayapa maeneo hayo hadhi ya kuwa Mikoa, hivo kuifanya Zanzibar kugawika katika Mikoa mitatu, Mikoa miwili Unguja na mmoja Pemba. Pia Zanzibar iligaiwa katika mudiriat 10 ambapo kwa Unguja 06 na Pemba 04, kwa wakati huo eneo la Mkoa mjini mMagharibi likijuulikana kwa jina la Mkoa Mjini ambao umegaiwa katika mudiriat ya Mjini na mudiriat ya shamba, baadae mudiriat zikaitwa Wilaya na viongozi waliitwa Wakuu wa Wilaya (Area Commission) .
Katika miaka ya 1970, Zanzibar iligaiwa katika Mikoa 04 ikijumuisha:-
1. Mkoa Mjini Magharibi
2. Mkoa wa Kusini
3. Mkoa wa Kaskazini
4. Mkoa wa Pemba
Ambapo Mkoa Mjini Magharibi uligaiwa katika Wilaya ya Mjini na Magharibi. Mikoa yote ya Zanzibar ukiwemo Mkoa Mjini Magharibi ilikuwa chini ya Ofisi ya Rais, kuanzia wakati wa Mapinduzi hadi ilipoanzishwa Ofisi ya Waziri |Kiongozi kwa toleo la tarhe 03 May
1984 la mabadiliko ya Wizara na Idara zake. Ofisi za Mikoa ukiwemo Mkoa Mjini Magharibi miaka ya 2000 wakati wa utawala wa Rais wa awamu ya tano Dk Salmin Amour Juma …….

Habari na Matukio