OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Katibu Tawala Mkoa wa Mjini Magharibi awafariji wahanga wa Moto
HabariHabari Mpya

Katibu Tawala Mkoa wa Mjini Magharibi awafariji wahanga wa Moto

Katibu Tawala Mkoa wa Mjini Magharibi  Nd. Mohammed Ali Abdalla ameambatana na Katibu Tawala Wilaya ya Mjini Dkt. Said Mrisho wakati wa kuwafariji Wahanga wa moto katika Nyumba za Wazee Sebleni na kuwajulia hali zao  zinavyoendelea.

Aidha wakati huo huo Katibu Tawala Mkoa wa Mjini ametembelea Nyumba ilioathirika na moto Kiponda na kutoa ushauri Shirika la Nyumba Zanzibar, Kamisheni ya Wakfu , Mamlaka ya Mji Mkongwe na  kufanya tathmini ya miundo mbinu ya Majengo hayo ili kudhibiti maafa.

Pia Sheha wa Shehia ya Kiponda Mh. Juma Khamis Makame amesema wakaazi wa Juu  wa jengo hilo wamepoteza mali na vifaa vyao vyote wakati wa mripuko huo, sambamba na hayo  ameeleza kuwa wakaazi wa kati na chini wa Jengo hilo wameibiwa vifaa na Thamani nyengine baada ya mripuko huo.

Jengo hilo lenye nambari ya usajili 1508 na 1509 lina Familia 16 wamepatiwa hifadhi ya Makaazi  katika Nyumba za Wazee Sebleni.