OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Historia

HISTORIA YA MKOA MJINI MAGHARIBI

Kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964 Zanzibar iligaiwa jiografia katika maeneo makubwa matatu yaliyopewa hadhi ya Wilaya ambayo ni :-

  • Wilaya ya Mjini
  • Wilaya ya Mashamba
  • Na Wilaya ya Pemba

Kutokana na hali hiyo Zanzibar baada ya Mapinduzi ikayapa maeneo hayo hadhi ya kuwa Mikoa, hivo kuifanya Zanzibar kugawika katika Mikoa mitatu, Mikoa miwili Unguja na mmoja Pemba. Pia Zanzibar iligaiwa katika mudiriat 10 ambapo kwa Unguja 06 na Pemba 04, kwa wakati huo eneo la Mkoa mjini mMagharibi likijuulikana kwa jina la Mkoa Mjini ambao umegaiwa katika  mudiriat ya Mjini na mudiriat ya shamba, baadae mudiriat zikaitwa Wilaya na viongozi waliitwa Wakuu wa Wilaya (Area Commission) .
Katika miaka ya 1970, Zanzibar iligaiwa katika Mikoa 04 ikijumuisha:-

  • Mkoa Mjini Magharibi
  • Mkoa wa Kusini
  • Mkoa wa Kaskazini
  • Mkoa wa Pemba

Ambapo Mkoa Mjini Magharibi uligaiwa katika Wilaya ya Mjini na Magharibi. Mikoa yote ya Zanzibar ukiwemo Mkoa Mjini Magharibi ilikuwa chini ya Ofisi ya Rais, kuanzia wakati wa Mapinduzi hadi ilipoanzishwa Ofisi ya Waziri |Kiongozi kwa toleo la tarhe 03 May 1984 la mabadiliko ya Wizara na Idara zake. Ofisi za Mikoa ukiwemo Mkoa Mjini Magharibi miaka ya 2000 wakati wa utawala wa Rais w awamu ya tano Dk Salmin Amour Juma zilikuwa chini ya wizara yta Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ hadi mwaka 2010 zilipopelekwa chini ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Katika kipindi cha mwaka 1980 Mkoa Mjini Magharibi ulikuwa na majimbo 13, ambapo majimbo 11 ya Wilaya ya Mjini na Majimbo 2 ya Wilaya ya Magharibi. Majimbo hayo yalikuwa yakiongozwa na wenye viti wa tawi la CCM wakati chama kiliposhika hatam kwa mfumo wa chama kimoja, ambao ni watendaji waliowakilisha Serikali hadi mwaka 1986 ulipoanzishwa mfumo wa kutenganisha uongozi wa chama na Serikali kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Mabadiliko makubwa Zaidi ya kutengenishwa Chama na Serikali yalitokea Juni 1992 ulipoanzishwa mfumo wa vyama vingi.
Baada ya Mapinduzi ya 1964 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi ilikuwa ikitumia jengo linalotumiwa na ZBC TV hivi sasa (Karume House) ambalo kabla ya Mapinduzi lilijuulikana kwa jina la Khalifa Holl katika miaka ya70, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi lilikuwa likitumia jengo la Majestic cinema na baadae Ofisi ya Mkoa na Wilaya ya Mjini ikahamia jengo la Manispaa (Baharmal building)  na baadae ilihamia jengo la Sanaa na Utamaduni Forodhani na katika mwaka 1991 Ofisi ilihamia Vuga hadi hii leo.
Wakuu wa Mikoa waliongoza Mkoa Mjini Magharibi na mwaka


Nam
Jina la KiongoziMwaka alioanzaMwaka aliomaliza
1Bw: Ali Mwinyi Gogo19641965
2Bw: Mdungi Usi1965
3Bw: Tawakal Khamis1969
4Bw: Saidi Washoto19691983
5Bw: Tahir Silima19831985
6Bw: Rajab Kheir Yussuf19851985
7Bw: Ame Mohamed1985
8Bw: Ramadhan Said
9Dk: Ishau Abdallah Khamis19901991
10Bw: Salum Juma Othman19911995
11Bw: Abdulla Rashid19951998
12Bw:Muhsin Ameir19982001
13Bw: Abdulla Mwinyi Khamis20012017
14Bw: Ayoub Mohammed Mahmoud20172019
15Bw: Hassan Khatib Hassan20192020
16Bw: Idrissa Kitwana Mustafa2020Hadi Sasa