OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Baraza la Biashara la Mkoa limeshauriwa kuziangalia sheria na kanuni zinazosimamia biashara
HabariHabari Mpya

Baraza la Biashara la Mkoa limeshauriwa kuziangalia sheria na kanuni zinazosimamia biashara

Baraza la Biashara la Mkoa Mjini Magharibi limeshauriwa kuziangalia sheria na kanuni zinazosimamia biashara ili kuepuka wafanya biashara wa jumla kujiingiza katika kufanya biashara za reja reja.

Wakichangia katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika Ofsi ya Mkuu wa Mjini Magharibi, Wajumbe wa baraza hilo wamesema kitendo cha wafanya biashara wa jumla kuuza rejereja kimekuwa kikiwaangusha wafanyabiashara wadogo wadogo kuendesha biashara zao.

Wamesema wafanyabiashara na wajasiriamali wengi wadogo wadogo biashara zao zimeanguka na baadhi kushindwa kulipa mikopo yao  kutokana na  wajeta wao walio wengi  kununua bidhaa  kwenye maduka ya rejereja ya  wafanya biashara wa jumla.

Aidha wameiomba Manispaa  kuweka maeneo ya maegesho ya gari na vyombo vya moto katika masoko ili kuepusha vyombo vya usafiri kuegeshwa mbele ya milango ya maduka hali inayopelekea wanunuzi kushindwa kununua bidhaa kwenye maduka hayo.

Kwa upande wake  Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Moh’d  Ali Abdalla amesema Mkoa utahakikisha unazishirikisha taasisi zote zinazohusika na biashara kwenye vikao hivyo ili kuweza kutoa ufafanuzi juu ya masuala yanayoibuliwa na wajumbe.

Ameongeza kuwa Mkoa utayafanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na wajumbe wa baraza hilo  ili  sekta ya biashara iweze kukua na kuimarika zaidi ndani ya Mkoa huo.