OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Wadau wa Demokrasia watakiwa kuondosha tofauti zao katika kuiletea maendeleo Zanzibar
HabariHabari Mpya

Wadau wa Demokrasia watakiwa kuondosha tofauti zao katika kuiletea maendeleo Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wadau wa Demokrasia kuondoa tafauti zao za kisiasa katika kujadili masuala ya maendeleo nchini.

Ameyasema hayo huko ukumbi wa Golden Tulip Hotel wakati akifungua mkutano wa kujadili masuala mahsusi ya Zanzibar yanayohusu Demokrasia ya vyama vingi vya kisiasa.

Amewataka wadau hao kuwa na dhamira nzuri wakati wa majadiliano hayo ili lengo la kukaa pamoja kwa liweze kupatikana

Aidha amewapongeza wadau wa vyama vya siasa, asasi za kirai na wafadhili wote kwa mashirikiano yao yaliyopelekea kufanikisha mkutano huo

Mkutano huo wa siku tatu unatarajiwa kufungwa tarehe 06/10/2022 na Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe. Othman Masoud Othman