OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Mtu mmoja afariki dunia katika ziwa la Jangamizini
HabariHabari Mpya

Mtu mmoja afariki dunia katika ziwa la Jangamizini

Mtu mmoja Mwanamme anaekisiwa kuwa na umri wa miaka 52 amefariki dunia baada kuzama katika Ziwa la Jangamizini liliopo mpakani mwa shehia ya Mambosasa na Chunga Wilaya ya Magharibi B Unguja

Daktari wa kitenge cha dharura cha Hospitali ya Mmnazi mmoja Asya Moh’d Suleiman amethibitisha kupokewa kwa mwili wa marehemu katika hospitali hiyo.

Mjumbe wa Sheha wa Shehia Rehema Iddi Hassan ameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni kuwa mtu huyo alikua akivuka katika Ziwa hilo na kuzama jambo lililopelekea kupoteza maisha

Tukio hilo lilitokea majira ya saa Saba (7 ) mchana Mwili umeonekana saa 10:29 alasiri