OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Mkuu wa Mkoa ameipongeza Taasisi ya JATA kwa nia yake ya kutatua changamoto za vijana
HabariHabari Mpya

Mkuu wa Mkoa ameipongeza Taasisi ya JATA kwa nia yake ya kutatua changamoto za vijana

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini jitihada zinazochukuliwa na wadau wa maendeleo katika kutatua changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo vijana.

Akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Jumuia ya Watanzania Waliosoma Japan (JATA),uliofanyika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Kilimani, amesema  juhudi zao hizo zimekuwa zikiisaidia Serikali katika kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo vijana.

Mkuu wa Mkoa ameipongeza JATA kwa kuamua mkutano wao wa mwaka huu kujadili suala la ongezeko kubwa la vijana kujiingiza katika vitendo vya uhalifu pamoja na kuishauri Serikali njia muafaka za kupambana  na tatizo hilo.

Amesema ajenda hiyo ina umuhimu wa kipeke na kuwapongeza JATA kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na changamoto za ongezeko la mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Amesema kwa kuatambua kuwa vijana kama wabia muhimu katika kuleta maendeleo Serikali ya Awamu ya Nane imeweka mazingira mazuri  ya kuwawezesha vijana kunufaika na fursa mbali mbali za ajira, elimu, ujasiriamali, mikopo nafuu na fursa nyenginezo.

Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kufungua mkutano huo, Mwenyekiti wa JATA Tanzania Gregory Mlay amesema mkutano huo utajadili changamoto ya ongezeko la vijana kujiingiza katika vitendo vya uhalifu na kuja na mapendekezo kwa Serikali.

Mwakilishi wa Shirika la Misaada la Japan (JICA) nchini Tanzania You Aoki amesema jumla ya watanzania 4,500 wakiwemo wazanzibari 472 wamepatiwa mafunzo na JICA katika kipindi cha miaka 60 ya mashirikiano yao na Tanzania.

Mkutano huo wa siku moja uliwashirikisha wajumbe wa JATA kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na waalikwa kutoka taasisi mbali mbali za Serikali uliwapa fursa pia kutembelea maeneo ya miradi, uzalishaji na vyuo vya mafunzo.