OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RC-Mjini Magharibi awapongeza wanafunzi wa Kidato cha sita kwa kupandisha ufaulu
HabariHabari Mpya

RC-Mjini Magharibi awapongeza wanafunzi wa Kidato cha sita kwa kupandisha ufaulu

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amewapongeza wanafunzi wa Mkoa  huo waliomaliza kidatu cha Sita mwaka 2022 kwa matokeo mazuri waliyopata katika mtihani wa taifa

Ametoa pongezi hizo katika mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu matokeo ya mtihani huo, ofisini Kwake Vuga

Amesema ufaulu wa mwaka huu ni bora zaidi ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita ambapo kiwango cha ufaulu kimefikia asilimia 99.89  wakati waliofeli ni asilimia 0.11

Amesema kati ya watahiniwa 2589 wanafunzi 519 wamepatiwa daraja la kwanza, 1,092 daraja la pili, 941 daraja la tatu, 32 daraja la nne na watahiniwa 5 pekee ndio walofeli

Kufuatia matokeo hayo Mkuu wa Mkoa amewapongeza pia Walimu, Wazazi, Wizara ya Elimu na wadau wote wa Elimu kwa mchango wao uliopelekea mafanikio ya wanafunzi hao.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amesema kwamba Mkoa wake unaendelea kutekeleza mikakati yake mbalimbali iliyojiwekea ili kupata matokeo mazuri ya mtihani wa taifa wa kidatu cha nne kwa mwaka huu.