OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Katibu Tawala Mkoa ahimiza wakandarasi wa miradi ya UVIKO-19
HabariHabari Mpya

Katibu Tawala Mkoa ahimiza wakandarasi wa miradi ya UVIKO-19

Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Mohd Ali Abdalla amewataka Wakandarasi wa miradi ya fedha za Uviko19 kufanya juhudi ya kumaliza miradi hiyo kama serekali ilivyoagiza 

Amesema licha ya hatua kubwa walizofikia bado wanatakiwa kuongeza bidii ili kukamilisha hatua iliyobakiza.

Katibu Tawala ametoa  agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa majengo ya wajasiriamali katika Wilaya ya  Mjini  , Magharibi A na Magharibi B

Akiwa ameambatana na Mafisa mbali mbali waandamizi wa Mkoa huo, Mohd amesema miradi hiyo itakapokamilika itawawezesha wajasiriamali kufanya kazi zao katika maeneo bora  zaidi.

Ameongeza pia ujenzi huo utaondoa changamoto inayowakabili wajasiriamali kwa kufanya biashara katika maeneo yasio rasimi.

Nae Muhandisi Msimamizi ndugu Salum Masoud  amesema ujenzi wa  majengo hayo umefikia asilimia tisini na unatarajiwa  kukamilika hivi karibuni 

Miradi aliokagua ni Majengo ya wajasiriamali Mombasa ,Welezo na Masumbani