OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Yatumieni mafunzo kuleta mabadiliko ya kiutendaji – RAS
HabariHabari Mpya

Yatumieni mafunzo kuleta mabadiliko ya kiutendaji – RAS

Wafanyakazi wa Afisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi wametakiwa kuyatumia mafunzo wanayoyapata kazini kuleta mabadiliko chanya katika utendaji wa kazi zao.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Moh’d Ali Abdalla alipokuwa akifunga mafunzo ya siku moja  kwa wafanyakazi wa Mkoa huo ili kuboresha utendaji wa kazi zao.

Amewataka wafanyakazi hao wa vitengo mbali mbali kuyafanyia kazi kwa vitendo mafunzo waliyopatiwa ili kuweza kufikia dhamira ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Katibu Tawala ameelezea matarajio yake kuwa mafunzo hayo yataleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwa wafanyakazi hao wa  Afisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi.

Aidha amesema Afisi itaendelea na utaratibu wa kuwapatia elimu wafanyakazi juu ya masuala mbali mbali ikiwemo suala la maadili ya kazi, mapambano dhidi ya rushwa na uhujumu uchumi, vitendo vya udhalilishaji na masuala mengine na kusema kuwa  Mkoa kama waratibu wa shughuli za Serikali lazima wayajue.

Kwa upande wao wafanyakazi  wameushukuru uongozi wa Afisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi kwa kuwapatia mafunzo hayo muhimu katika utekezaji wa kazi zao.

Wamesema mafunzo hayo yameweza kuwajengea uelewa mkubwa  kuhusu sheria na taratibu mbali mbali wanazopaswa kuzizingatia katika utekelezaji wa majukumu yao.

Semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Afisi ya Mkuu Mkoa ilishirikisha maofisa waandamizi, wakuu wa vitengo, maofisa na wafanyakazi wa sekta mbali mbali