OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Tawala  yatwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi
HabariHabari Mpya

Tawala  yatwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi

Mabingwa wa mpira wa miguu wa mashindano yanayoshindanisha timu za Wizara, Mashirika na Taasisi za Serikali timu ya Tawala imekabidhiwa rasmi kombe la mashindano hayo.

Tawala alikabidhiwa kombe hilo jana baada ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Veterans na kushinda goli 3-2 mchezo uliopigwa uwanja wa Mao ze Dong.

Timu ya Tawala ilitawadhwa mabingwa wa mashindano hayo baada ya timu ya Hospitali ya Kivunge kutoka Mkoa Kaskazini Unguja kuingia mitini katika mchezo wa fainali uliokuwa uchezwe jumapili iliyopita.

Tawala walifika uwanja wa Amani kuchezo fainali hiyo hata hivyo timu ya Kivunge hawakufika uwanjani na Kamati inayosimamia mashindao hayo kuwapa ubingwa Tawala.

Fainali ya kumpata bingwa wa  Zanzibar wa kombe la Mapinduzi kwa Wizara, Mashirika na Taasisi za Serikali itapigwa siku ya Jumapili katika uwanja huo huo wa Mao ze Dong kati ya bingwa wa Unguja Tawala na bingwa  kutoka Pemba Wizara ya Afya.