OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RAS: Aitaka Kamati ya Mitihani ya Mkoa Kutimiza Wajibu Wao
HabariHabari Mpya

RAS: Aitaka Kamati ya Mitihani ya Mkoa Kutimiza Wajibu Wao

Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Moh’d Ali Abdalla ameitaka Kamati ya Mitihani ya Mkoa huo kusimamia vyema mitihani ya taifa ya kidatu cha nne ambayo imeanza kufanyika mwanzoni mwa wiki hii.


Agizo hilo amelitoa katika kikao chake na kamati hiyo kutathmini namna mitihani hiyo inavyoendelea katika Mkoa Mjini Magharibi.

Akizumgumza na wajumbe wa Kamati hiyo Moh’d amewaeleza kuwa Taifa linawaamini, hivyo wanawajibu wa kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi hadi kukamilika kwake.

Amesema kwamba Mkoa usingependa kuona kunajitokeza kasoro zozote katika zoezi hilo ndani ya Mkoa wake.