OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>“Darajani souk Biashara masaa 24” Dkt. Mwinyi
HabariHabari Mpya

“Darajani souk Biashara masaa 24” Dkt. Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua rasmi mradi wa ujenzi wa maduka 452 wa Darajani Souk.

Akizungumza na hadhara iliyohudhuria hafla hiyo Dkt. Mwinyi amepongeza mashirikiano yaliyooneshwa na Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi na Chama cha Mapinduzi katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo.

Aidha amewataka watakaosimamia mradi huo pamoja wafanyabiashara watakaokodishwa milango kuhakikisha wanaitunza na kufanya matengenezo pale panapotokea hitilafu badala ya kuacha kuendelea kuharibika.

Amesema pia kituo hicho cha biashara kitakuwa na ulinzi na miundo mbinu ya taa na kuwataka wafanyabiashara kufanya biashara zao masaa 24.

Naye Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa ametoa shukurani za wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa huo kwa Rais wa Zanzibar kwa kufanikisha mradi huo.

Amesema kuwa Serikali ya Mkoa itaendeleza mashirikiano na sekta mbalimbali, wawekezaji na wakandarasiili kuona miradi iliyokusudiwa kutekelezwa katika Mkoa Mjini Magharibi inafanikiwa.