OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Mwenge wa Uhuru umeingia Wilaya ya Magharibi ‘A kuendelea na mbio zake.
HabariHabari Mpya

Mwenge wa Uhuru umeingia Wilaya ya Magharibi ‘A kuendelea na mbio zake.

Viongozi wa Wilaya ya Mjini wametakiwa kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Wilaya yao.

Agizo hilo limetolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Adallah Shaib Kaimu wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Mjini kwenda Wilaya ya Magharibi ‘A’ hapo Maruhubi.

Amewaeleza viongozi hao kuwa wana wajibu wa kusimamia kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Aidha amewataka pia kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi mapana ya wananchi wa Wilaya hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka amewashukuru viongozi wakuu wa nchi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi  kwa  mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wao.