OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>“Fanyeni mazoezi, kuleni vyakula vyenye virutubisho”-Mama Mariam Mwinyi
HabariHabari Mpya

“Fanyeni mazoezi, kuleni vyakula vyenye virutubisho”-Mama Mariam Mwinyi

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa jamii kuzingatia suala la Usalama wa Chakula kwani maradhi yatokanayo na chakula yamekuwa yakiongezeka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula ambavyo si salama kusababisha kuathiri afya za wananchi.

Ameyasema hayo leo tarehe 07 Juni 2023 katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama wa Chakula Duniani yaliyoanza kwa matembezi ya kilomita tano kuanzia Ofisi za Makao makuu ya ZFDA Mombasa hadi Mapinduzi Square (Kisonge), Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Mama Mariam amesema kula vyakula vyenye virutubisho, kilicho safi ni mtindo bora wa kula pamoja na kufanya mazoezi ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kutibu maradhi mbalimbali yatokanayo na mlo usiotimia.

Vilevile kwa kuzingatia kula mlo uliotimia wenye makundi maalumu ya vyakula bora ikiwemo mbogamboga, matunda, kunde, karanga, mbegumbegu , jamii ya wanyama na mazao ya baharini, nafaka , mzizi , ndizi mbichi na mafuta kwa afya bora kwa Watoto, Wazee na Wajawazito ili kuimarisha na kuweka mfumo imara wa kinga mwilini.