OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Mkutano wa Mkuu wa Mkoa na Wananchi wa Bububu Meli nane
HabariHabari MpyaUncategorized

Mkutano wa Mkuu wa Mkoa na Wananchi wa Bububu Meli nane

SERIKALI ya Mkoa Mjnini Magharibi imeswaagiza masheha wa mkoa huo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yako kwa kufuata shehria,taratibu na miongozo ya nchi katika kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi.

Hayo yameelezwa na mkuu wa Mkao Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa wakati akizungumza na wananchi wa shehia za Kikaangoni na Kihinani ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kutatua changamoto za wananchi katika shehia zao.

Amesema  wananchi kupatiwa huduma bila ya ubaguzi hivyo viongozi hao wanawajibu kufanya kazi zao kwa uadilifu ili kuhakikisha changamoto zinazowakabili wanachi hususani wanyonge zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi akizungumza na Wananchi wa Shehia ya Bububu Meli nane

“ Serikali hii ya awamu ya nane kipaumbele chetu ni kuwaondolea kero wananchi wetu na kuwaletea maendeleo,sasa katika mkoa huu wa Mjini Magharibi hakuna nafasi kwa kiongozi yeyote kumkosesha huduma ya msingi mwananchi”alisema Kitwana.

Aidha mkuu wa akizungumzia kuhusu vitendo vya udhalilishaji amewata wazazi na walezi kurudi katika utamaduni wa malezi ya zamani,ya malezi ya pamoja ili kuona vitendo hivyo vinaondoka.

Wananchi wakitoa malalamiko kwa Mkuu wa Mkoa

“ Katika mikutano yetu hii tumekua tukipata malalamiko mingi kuhusu vitendo vya uhalifu wa ukabaji na unyang’anyi kwa baadhi ya vijana wetu,sasa ninalowaomba wazazi wenzangu turudi katika utamaduni wetu wa asili wa kizanzibari wa malezi ya pamoja”alisema mkuu wa Mkoa.

Nao wananchi wa shehia za Kikaangoni na Kihinani wameuomba uongozi wa serikali ya mkoa kuendelea kuwaondoshea matatizo yanayowakabili ikiwemo vitendo vya kihalifu,udhaklilishaji,upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama pamoja na mfumko wa bei ya vifaa vya ujenzi na vyakula.

Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” akitoa ufafanuzi juu ya changamoto zinazowakabili Wananchi

“ Mheshimiwa mkuu wa Mkoa tunaomba sana wananchi wenu tumekuwa na chanagamoto nyingi zinatukabili katika shehia zetu,lakini chanagamoto kubwa kwa sasa ni mfumko wa bei kwa bidhaa mbali mbali tumekuwa hatuna uhakika na mlo wa kawaida” walisema baadhi ya wananchi hao.