OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Mkoa kuimarisha ukusanyaji mapato
HabariHabari Mpya

Mkoa kuimarisha ukusanyaji mapato

Matumizi ya mfumo wa ukusanyaji mapato ya Serikali kupitia ZanMalipo yatapelekea kuongeza  mapato yanayokusanywa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi pamoja na Wilaya zake.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Moh’d Ali Abdallah alipokuwa akifunga mafunzo kwa maofisa watakaosimamia mfumo huo wakiwemo wahasibu, washika fedha na maofisa tehama wa Mkoa na Wilaya.

Amesema kuwa atahakikisha vifaa vyote vinavyohitajika vinapatikana ili mfumo huo uanze kutumika mara moja.

Kwa upande wao maofisa hao wameeleza kuwa kuja kwa mfumo huo kutawawezesha wananchi kuwa na uhakika wa malipo wanayostahiki kulipa juu ya huduma mbali mbali zinazotolewa na Mkoa pamoja na Wilaya zake

Awali Ofisa kutoka Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar, Hawa Omar Salim alitoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huo wa ZanMalipo kwa maofisa hao kutoka Mkoa, Wilaya ya Mjini, Magharibi A na B.