OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Dk. Mwinyi afutarisha wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi.
HabariHabari Mpya

Dk. Mwinyi afutarisha wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, mwezi 17 Ramadhani alijumuika na wananchi  wa Mkoa Mjini Magharibi katika chakula cha futari iliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, Kikwajuni.

Katika hafla hiyo makundi maalum wakiwemo walemavu, yatima na wajane walijumuika kufutari pamoja na Rais wa Zanzibar.

Aidha Dk. Mwinyi alikabidhi sadaka ya vyakula pamoja na Misahafu kwa wananchi waliohudhuria katika shughuli hiyo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi, watendaji na wafanyakazi wa Mkoa Magharibi pamoja  na taasisi mbali mbali.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa alimshukuru Rais wa Zanzibar kwa kuandaa tafrija hiyo katika Mkoa wake na kuftari pamoja na wananchi.

Amesema kitendo hicho kimeonesha ni kwa kiasi gani Rais wa Zanzibar alivyo na moyo wa upendo kwa wananchi wake.