OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Changamkieni fursa za ujasiriamali: Abdallah Kaimu
HabariHabari Mpya

Changamkieni fursa za ujasiriamali: Abdallah Kaimu

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Abdallah Shaib Kaim ametoa wito kwa wanawake na vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya ujasiriamali.

Wito huo ameutoa wakati akitembelea mabanda ya wajasiriamali kuangalia bidhaa zao pamoja na shughuli za taasisi mbali mbali za serikali na binafsi huko Regeza mwendo, Wilaya ya Magharibi ‘A’.

Amesema kwamba kupitia ujasiriamali zipo fursa nyingi ambazo endapo watazitumia vizuri wataweza kujiajiri wenyewe na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.
Aidha amewahakikishia wajasiriamali hao kuwa Serikali zote mbili zitaendelea kuwawekea mazingira mazuri ili kuikuza sekta hiyo na kuwawezesha wananchi wengi zaidi kujiajiri wenyewe.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’ Susan Kunambi amemweleza Kiongozi wa Mbio za Mwenge kwamba Serikali imekuwa ikiwaunga mkono wajasiriamali kwa kuwapatia mikopo na masoko ya kuuza bidhaa wanazozalisha.