OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Dk. Mwinyi akitoa Msaada wa futari kwa watu wenye ulemavu, mayatima, wajane na wanaoishi mazingira magumu
HabariHabari MpyaHabari Picha

Dk. Mwinyi akitoa Msaada wa futari kwa watu wenye ulemavu, mayatima, wajane na wanaoishi mazingira magumu

Jumla ya wananchi elfu tatu wa Mkoa Mjini Magharibi wamepatiwa sadaka ya  bidhaa mbali mbali za chakula kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.        

Akikabidhi sadaka hiyo hapo uwanja wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michenzani, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi aliwashukuru watu mbali mbali waliojitolea kusaidia wananchi katika kipindi hiki.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amesema kuwa sadaka hiyo imetolewa kwa watu mbali mbali wa makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu na wenye  mazingira magumu.           

Aidha Mkuu wa Mkoa alimshkuru Rais wa Zanzibar kwa kukabidhi sadaka hiyo kwa wananchi wa Mkoa wake.       

Nao vilevile wananchi waliopokea sadaka hiyo walimshukuru Rais wa Zanzibar na kumuomba kuendeleza utamaduni huo mzuri kwa miaka ijayo.                            

Katika tukio hilo wananchi kutoka Wilaya tatu za Mkoa Mjini Magharibi walipokea  sadaka ya mchele, unga wa ngano, sukari, maharage na njugu mawe kwa niaba ya wananchi wengine.