OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Maofisa Habari, Uhusianao na Tehama watakiwa kutoa taarifa.
HabariHabari Mpya

Maofisa Habari, Uhusianao na Tehama watakiwa kutoa taarifa.

Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Moh’d Ali Abdalla amewataka Maofisa habari, uhusiano na tehama  kutoa taarifa kupitia vyombo mbambali vya habari juu mambo yanayotekelezwa na Serikali ndani ya Mkoa huo.

Agizo hilo amelitoa katika kikao chake na  maofisa hao kutoka Mkoa, Wilaya, na Manispaa za   Mkoa Mjini Magharibi kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Vuga.

Amewaeleza Maofisa hao kuwa Mkoa kwa kushirikiana na Wilaya na Manispaa itazifanyia kazi changamoto zinazowakabili ili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi Zaidi.

Kwa upande mwengine Katibu Tawala amewapongeza kwa utendaji wao wa kazi licha ya uhaba wa vitendea kazi unaowakabili na kuwataka waongeze juhudi zaidi za kuwafikishia habari wananchi wa Mkoa huo.

Nao Maofisa hao wamemuomba Katibu Tawala kuzipatia ufumbuzi changamoto mbali mbali ambazo zinakwamisha utendaji wao wa kazi.

Kikao hicho ni mfululizo wa vikao vya Katibu Tawala kukutana na watendaji wa Vitengo mbali mbali kuzungumzia namna ya kuboresha utendaji wa kazi za Mkoa huo.