OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Sola kupunguza tatizo  la umeme zanzibar – RC Idrissa
HabariHabari Mpya

Sola kupunguza tatizo  la umeme zanzibar – RC Idrissa

Mkuu wa Mkoa  wa Mjini  Magharibi Mheshimiwa Idrissa Kitwana Mustafa amesema uwepo wa umeme  wa Sola atasaidia kupunguza changamoto zilizopo za umeme  wa kawaida.

Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo huko Gulioni katika ghafla ya uzinduzi wa mradi wa Sola Maisha Bora wakati alipokua akitoa salamu za wananchi wa Mkoa wake.

Amesema umeme ni uhai na ni maisha Bora yenye kujenga uchumi na ustawi wa  watu ambapo sehemu ambayo haina umeme  hakuna maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hivyo ujio  wa umeme  huo  wa Sola atasaidia kupunguza tatizo liliopo la umeme ndani ya Mkoa wa mjini Magharibi  na Zanzibar kwa ujumla.

Aisha Mheshimiwa Idrissa amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa juhudi zake za kuwaletea Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar.