OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Wafanyakazi Mkoa Mjini Magharibi wapongezwa kwa kuanzisha timu ya mprira wa miguu
HabariHabari Mpya

Wafanyakazi Mkoa Mjini Magharibi wapongezwa kwa kuanzisha timu ya mprira wa miguu

Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibu Mohamed Ali Abdalla amewapongeza wafanyakazi wa Mkoa huo kwa uamuzi wao wa kuunda timu ya mpira wa miguu ya Mkoa.

Akizungumza na wafanyakazi hao hapo Afisi ya Mkuu Mkuu wa Mkoa Vuga, amesema uongozi wa Mkoa upo tayari kuunga mkono na kuipa kila aina ya mshirikiano timu hiyo ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Amesema kuundwa kwa timu ya mpira wa miguu ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mkoa kumemshawishi kuona Wilaya na Manispaa za Mkoa Mjini Magharibi nazo zinaunda timu zao ili kuanzisha mashindano ya Mkoa.

Aidha Mohamed amewataka viongozi wa timu kuendelea na nyadhifa zao hadi pale utakaponyika uchaguzi rasmi wa kuchagua viongozi na kuahidi kuwa hautachukua muda mrefu kufanyika.Kiongozi wa Timu Ali Abdalla Natepe amesema matumaini yao ni kuifanya timu ya Mkoa Mjini Magharibi kuwa moja ya timu bora zitakazoshiriki mashindano mbali mbali yanayoshirikisha taasisi za Serikali.

Amesema tayari timu hiyo imeshacheza mechi kadhaa za kirafiki na imeonesha uwezo mkubwa wa kucheza na kuleta ushindani kwenye mashindano yanayofanyika Zanzibar na Tanzania Bara.

Naye mhamasishaji wa timu Said Kombo Ali (Van Star), amesema kitendo cha uongozi wa Mkoa kuiunga mkono timu hiyo wataweza kupiga hatua kubwa siku za usoniAmesema kwa sasa timu inakabiliwa na ukosefu wa vifaa mbali mbali vya michezo pamoja na usafiri wakati wanapokwenda kucheza mechi kwenye viwanja tofauti.

Kwa upande wake Afisa Utumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Maryam Saad amesema mazoezi ni afya hivyo ameeleza haja ya wafanyakazi wanawake nao kushiriki katika michezo mengine ili kujenga afya zao.