OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RC Kitwana alitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa uweledi na uwadilifu
HabariHabari Mpya

RC Kitwana alitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa uweledi na uwadilifu

Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amewataka wapiganaji wa Jeshi la Polisi mkoani humo kufanya kazi kwa uweledi na uwadilifu mkubwa ili kuweza kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao

Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo huko katika ukumbi wa mkutano wa Ziwani Polisi wakati alipokua akizungumza na viongozi na wapiganaji hao katika mkutano maalum wa tathmini ya utekelezaji wa kazi za Jeshi hilo ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema Jeshi la Polisi linaaminiwa sana katika kulinda raia na mali zao hivyo ni wajibu wa askari wa jeshi hilo kutekeleza vyema kazi zao kwa uwadilifu, nidhamu na mashirikiano makubwa ili kuendelea kujenga imani kwa wananchi.

Mkuu huyo wa Mkoa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo amesema heshima kubwa inayopatikana ndani ya mkoa huo inatokana na hali bora ya ulinzi na usalama inayosimamiwa na jeshi la polisi kwa mashirikiano ya karibu na vikosi vya SMZ. Katika utekelezaji wa majukumu na kazi zao za kila siku.

Aidha amewataka makamanda wa polisi wa Wilaya, wakuu wa vituo vya polisi na maafisa waliopo katika ngazi za Shehia wa jeshi hilo kuendeleza juhudi zao kwa mashirikiano ya karibu na masheha ili kupambana na wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani katika shehia.

Kadhalika amewataka askari hao kutojihusisha na matendo yanaoenda na kinyume na maadili ya kazi za jeshi hilo ikiwemo upokeaji wa rushwa kwani kufanya hivyo kutaondoshea heshima askali hao pamoja na jeshi hilo kwa ujumla.

Katika hatua nyengine Idrisaa amealeza kusikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu kufanya matukio ya uhalifu ikiwemo kupiga wananchi na askari wa jeshi hilo jambo ambapo halitofumbiwa macho kwa kuhakikisha kuwa hatua za kisheria zitachukulia kwa wale wanaohusika na matendo hayo.

Mapema akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini magharibi Richard Tadeo Mchomvu amesema Jeshi la Polisi litaendelea na juhudi zake za kuhakikisha kuwa amani na utulivu inaendelea kudumu ndani ya mkoa huo.

Akitoa shukrani kwa niamba ya askari wenzake kamanda wa polisi wilaya ya Magharibi ‘A’ OCD Mary Joseph Sungi ameeleza kuwa tayari kuyafanyia kazi maelekezo yote huku akikakikishia kudumisha nidhamu na uwajibikaji.