OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Mwenge wa Uhuru waanza mbio zake Mkoa Mjini Magharibi.
HabariHabari Mpya

Mwenge wa Uhuru waanza mbio zake Mkoa Mjini Magharibi.

Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake katika Mkoa Mjini Magharibi ukitokea Mkoa wa Dar-es-salaam.

Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yalifanyika katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume ambapo Mkuu wa Mkoa Dar-es-salam Albert Chalamila aliukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa.

Mara baada ya makabidhiano  hayo, Mkuu wa Mkoa aliukabidhi Mwenge wa Uhuru  kwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka ili kuanza mbio zake katika Wilaya hiyo.

Jumla ya miradi 21 yenye dhamani ya zaidi ya shilingi bilioni 118 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya tatu za Mkoa Mjini Magharibi.

Mwenge wa Uhuru utaendelea na mbio zake kesho Jumanne katika Wilaya ya Magharibi ‘A’,  siku ya Jumatano katika Wilaya ya Magharibi ‘B’ na Alkhamis tarehe 1 Juni utakabidhiwa  Mkoa wa Kusini Unguja.