OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Serikali haitamvumilia mtendaji yoyote atakaechelewesha malipo kwa Kampuni zinazojenga miradi ya maendeleo kupitia fedha za UVIKO 19.
HabariHabari Mpya

Serikali haitamvumilia mtendaji yoyote atakaechelewesha malipo kwa Kampuni zinazojenga miradi ya maendeleo kupitia fedha za UVIKO 19.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema haitamvumilia mtendaji yoyote atakaechelewesha malipo kwa Kampuni zinazojenga miradi ya maendeleo kupitia fedha za UVIKO 19.

Indhari hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdallai kufuatia malalamiko ya Kampuni ya Ujenzi ya ESTIM inayojenga Skuli ya Msingi ya ghorofa 3 huko Mwanakwerekwe. Akiwa katika ukaguzi wa ujenzi wa Skuli hiyo wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Magharibi B, Makamu wa Pili wa Rais amezitaka Wizara ya Fedha na Mipago na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhakikisha inailipa Kampuni hiyo haraka iwezekanavyo ili iweze kuendelea na ujenzi wa mradi huo. Amesema kila pande ina wajibu wa kuheshimu mkataba kwa upande wake likiwemo suala la Serikali kufanya malipo ya wajenzi kwa wakati.

Wakati huo huo Mhe. Hemed ameiagiza Wizara ya Elimu kuajiri mshauri elekezi ili aweze kusimamia ujenzi wa miradi yao. Amesema miradi iliyo chini ya Wizara hiyo ni mikubwa, hivyo ni lazima wawe na mtaalamu huyo ili kuhakikisha miradi hiyo ya Serikali inajengwa kwa viwango vinavyotakiwa.

Kwa upande wao watendaji wa Sekta hizo walimueleza Makamu wa Pili wa Rais juu ya changamoto mbali mbali zilizopelekea kuchelewa kufanya malipo kwa Kampuni hiyo. Awali Mkandarasi wa ESTIM lieleza kuwa Kampuni yake imekuwa ikicheleweshewa malipo licha ya kukabidhi cheti cha ujenzi kwa wakati.