OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Tawala FC yatinga Nusu Fainali Mapinduzi Cup
HabariHabari Mpya

Tawala FC yatinga Nusu Fainali Mapinduzi Cup

Timu ya Wizara ya Nchi (AR) Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ imefanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la Mapinduzi baada ya kuibwaga mabao 2-1 timu ya Wizara  ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo

Ilichukua dakika 27 tu ya kipindi cha kwanza kwa mchezaji Yussouf Fadhil kutingisha nyavu za Wizara ya Habari katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Mao ze dong.

Dakika 5 baadae Yussouf Fadhil alifunga bao la pili baada ya kuichambua ngome ya timu ya  Wizara ya Habari na kuachia shuti kali lililoenda moja kwa moja hadi nyavuni.

Wizara ya Habari iliamka kipindi cha pili na kuweza kupata bao kwenye dakika ya 53 lililodumu hadi mwisho wa mchezo

Kufuatia ushindi huo, Timu ya Wizara ya Nchi (AR) Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ inayoshiriki mashindano ya Kombe Mapinduzi kwa Timu za Wizara na Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itacheza na timu ya Wizaya ya Nchi (AR) fedha na Mipango katika mchezo wa nusu fainali.

Awali Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Moh’d Ali Abdalla aliwaeleza wachezaji hao kwamba atatoa zawadi kwa kila mchezaji atakaefunga goli pamoja na timu endapo watashinda mechi hiyo ya robo fainali ya kombe la  Mapinduzi kwa timu ya Wizara na taasisi za SMZ