OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Maafisa utumishi fanyeni kazi kwa uzalendo na uweledi – Waziri Haroun
HabariHabari Mpya

Maafisa utumishi fanyeni kazi kwa uzalendo na uweledi – Waziri Haroun

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala bora Mhe Haroun Ali Suleimani amewataka Maafisa Utumishi wa Mkoa  Mjini  Magharibi kuwa wazalendo na kuacha maslahi binafsi katika utendaji wao wa kazi .

Mhe .Haroun amesema hayo katika ukumbi wa Afisi ya Mkuu wa Mkoa  Mjini Magharibi wakati wa ufunguzi wa mafunzo  ya usimamizi wa Rasilimali watu katika Utumishi wa umma.

Amesema kuwa ni vyema kwa viongozi hao kufanya kazi kwa uweledi na kujali wakati katika utendaji jambo ambalo litaleta maendeleo mazuri kiutendaji.

Mhe . Haroun amesema viongozi hao wanawajibu wa kutoa maamuzi sahihi kwa kuangalia maslahi ya wafanyakazi na kufuatilia hatua kwa hatua utendaji wa wafanyakazi hao.

Aidha amewaomba kufuata vyema sheria na kanuni za kiutumishi kwa kufuata utaratibu wa kupanga ratiba  za kazi zao.

Nae Katibu Tawala Mkoa huo Mohamed Ali Abdallah amesema lengo la mafunzo hayo ni kusimamia sheria na kanuni za utumishi wa umma ili kuweza kutoa huduma bora kwa wataka huduma na kuleta matokeo chanya.

Aidha amesema Mkoa wake utahakikisha unasimamia  misingi ya sheria na taratibu bila kumuonea mfanyakazi yoyote na kuahidi kuwa mara baada ya mafunzo hayo uongozi wa Mkoa huo utaandaa utaratibu wa kukutana na Viongozi Wilaya, Mabaraza ya Manispaa Pamoja na maafisa Utumishi kwa lengo la kusimaimia uwajibikaji.

Akitoa mada juu ya maadili ya watumishi wa umma Afisa mafunzo kutoka Afisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala bora Khamisi Haji Ngwali amesema lengo la Serikali katika utendaji wa kazi kwa taasisi ni kufuata sheria zote na kanuni zitakazomuongoza mtendaji na kujitathmini katika kutimiza wajibu pamoja na kuacha kufanya kazi kwa mazowea ili kuleta maendeleo katika Serikali  na jamii kwa ujumla.