OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RC atoa wiki 2 kutekelezwa makubaliano
HabariHabari Mpya

RC atoa wiki 2 kutekelezwa makubaliano

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa ametoa muda wa wiki mbili kutekelezwa makubaliano yaliyofikiwa baina ya Shirika la Bandari Zanzibar na wachukuzi katika bandari ya Majahazi Malindi Funguni.

Amesema kuwa Mkoa hauna pingamizi na makubaliano hayo hasa ikizingatiwa kuwa yamefikiwa na wachukuzi wenyewe pamoja na Shirika la Bandari.

Akizungumza na viongozi wa pande mbili za wachukuzi  wenye mgogoro na watendeji wa Shrika la Bandari katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Vuga, Idrissa amesema Mkoa hautegemei kuona makubaliano waliyofikia  wanashindwa kuyatekeleza.

Aidha ametoa indhari kuwa endapo mgogoro huo utaendelea bandari hiyo itafungwa ili kuepusha uvunjifu wa amani.

Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa amelitaka Shirika la Bandari kusimamia utekelezaji wa makubaliano hayo na kumpa taarifa juu ya hatua itakayofikiwa ndani ya muda aliyoutoa.

Awali watendaji wa Shirika la Bandari walimweleza Mkuu wa Mkoa kuhusu juhudi walizochukua kupatanisha mgogoro huo wa muda mrefu hata hivyo wachukuzi hao wameshindwa kukubaliana.

Bandari ya Funguni imekuwa ikitumiwa na Majahazi yanayoshusha mbao na miti ya kujengea kutoka Tanzania Bara.