OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi itahakikisha wawekezaji ndani ya Mkoa wanatimiza wajibu wao
HabariHabari Mpya

Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi itahakikisha wawekezaji ndani ya Mkoa wanatimiza wajibu wao

Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi imesema kwamba itahakikisha wawekezaji ndani ya Mkoa huo wanatimiza wajibu wao wa kusaidia  huduma muhimu za jamii ziliyopo karibu na miradi yao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Maghribi Idrissa Kitwana Mustafa katika kikao cha Baraza la Biashara la Mkoa huo kilichofanyia Ofisini kwake Vuga kujadili mambo mbali mbali yanayohusu biashara.

Amesema kwamba bado kuna mwamko mdogo wa wawekezaji kusaidia huduma za jamii katika Mkoa wake, hivyo Mkoa utakaa pamoja na wawekezaji waliyowekeza kwenye Mkoa huo ili kuwashajiisha kutoa michango yao kama sheria zinavyoelekeza.

Amesisitiza kuwa kwa vile suala la wawekezaji kusaidia huduma za jamii lipo kisheria, Mkoa  utafatilia kwa karibu  ili kuona wawekezaji ndani ya Mkoa huo wanatoa mchango wao kusaidia miradi  mbali mbali ndani ya Mkoa wake.

Mkuu wa Mkoa ametaja maeneo mbali mbali ikiwemo sekta ya afya, elimu na miundo mbinu mengine huduma zake zitaweza kuimarika zaidi endapo wawekezaji na  taasisi nyengine watatoa michango yao ipasavyo katika kuimarisha huduma hizo.

Kwa upande wao wajumbe wa Baraza hilo wameomba kuzipatia ufumbuzi changamoto ziliyopo kwa  baadhi ya Taasisi za Serikali zinazopelekea kukwamisha wawekezaji kusaidia huduma za jamii. Aidha wameshauri Baraza hilo kukutana na vyombo vinavyohusika na ukusanyaji wa kodi ili kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabishara katika ulipaji wa kodi mbali mbali za Serikali