OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu awataka wajasiriamali kuwa wavumilivu wakisubiri vifaa vya boti walizokabidhiwa
HabariHabari Mpya

Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu awataka wajasiriamali kuwa wavumilivu wakisubiri vifaa vya boti walizokabidhiwa

Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu imevitaka vikundi vya wajasiriamali waliopewa boti za uvuvi kuwa wastahamilivu wakati Wizara hiyo iko mbioni kuwapatia vifaa vyengine kwa ajili ya kazi zao.

Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu Dkt. Aboud Suleiman Jumbe katika kikao kilichofanyika Afisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi kilichowashirikisha wajasiriamali hao pamoja na Uongozi wa Mkoa huo.

Amevitaka vikundi hivyo kuorodhesha vifaa ambavyo bado  baadhi yao hawajapatiwa ili waweze kupatiwa vifaa hivyo.

Aidha Dkt.Aboud amewataka pia kupeleka maombi  yao katika Wizara yake kabla ya kupeleka katika taasisi nyengine ya Serikali.

Awali wajasiriamali hao walieleza kuwa licha ya kupatiwa boti za uvuvi hata hivyo bado wameshindwa kuanza kuzitumia kutokana na ukosefu wa vifaa mbali mbali wanavyohitaji kwa kazi zao za uvuvi

Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi  Mohammed Ali Abdalla ameushukuru uongozi wa  Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu kwa kuweza kukutana na vikundi hivyo ili kuyapatia ufumbuzi mahitaji yao.