OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akikagua miradi inayojengwa na fedha za Uviko519
Habari

Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akikagua miradi inayojengwa na fedha za Uviko519

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema hatua ya ujenzi wa hospitali 11 kwa kila Wilaya ni sehemu ya Mapinduzi makubwa ya sekta ya afya Zanzibar.


 Amesema hayo leo Julai 16 mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Magharibi A, Shehia ya Mbuzini katika Ziara ambayo imeanza leo ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoa wa Mjini Magharibi.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameitaka kampuni ya MEGHA Engineering and Infrastructure (MEIL) kukabidhi mradi wa maji unaojengwa Shehia ya Kidichi ifikapo Januari mwaka 2023 kama walivyohaidi. 
Amesema hayo leo Julai 16 wakati akikagua mradi wa maji unaojengwa na kampuni hiyo  katika Ziara ambayo imeanza leo ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Mjini Magharibi.