OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Masheha watakiwa kuwatambua wahamiaji  
HabariHabari Mpya

Masheha watakiwa kuwatambua wahamiaji  

Masheha wa Mkoa Mjini Magharibi wametakiwa kufuatilia kwa karibu watu wanaohamia kwenye Shehia zao ili kudhibiti wahamiaji haramu.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo masheha katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Magufuli  iliyoandaliwa na ldara ya Uhamiaji ya Mkoa huo.

Amewaeleza kuwa kumekuwa na wimbi la wageni wanoingia kwenye mkoa huo kutoka nchi za jirani, hivyo ni vyema kuwatambua na kutoa taarifa dhidi ya watu wenye mashaka nao.

Aidha Mkuu wa Mkoa ameishukuru ldara ya Uhamiaji kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yataongeza uelewa wa masheha kuhusu masuala ya uhamiaji na  kuwaomba yawe endelevu.

Kwa upande mwengine Idrissa amewataka masheha kuhakikisha wanadhibiti uuzaji holela wa ardhi dhidi ya wageni kwenye maeneo yao.

Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kufungua semina hiyo, Msaidizi Kamishna wa Idara Uhamiaji ambae pia ni Afisa Uhamiaji wa Mkoa Mjini Magharibi Ramadhan Khamis Makame amesema semina hiyo itawawezesha masheha kupata uelewa juu ya masuala mbali mbali yanayohusu uhamiaji.

 Mada nne zimewasilishwa kwenye semina hiyo ikiwemo huduma zinazotolewa na Ofisi ya uhamiaji ya Mkoa, uraia, wahamiaji haramu na nafasi za masheha katika huduma za kiuhamiaji.