OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Wizara ya Biashara na maendeleo ya viwanda yapongezwa kwa kuboresha maonesho ya Biashara
HabariHabari Mpya

Wizara ya Biashara na maendeleo ya viwanda yapongezwa kwa kuboresha maonesho ya Biashara

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Wizara ya Biashara na maendeleo ya viwanda kwa kuboresha  Maonesho ya Tisa Biashara ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.

Mhe. Hemed ameyasema hayo alipotembelea Maonesho hayo kujionea shughuli zinazofanywa na washiriki mbali mbali wa monesho hayo. Amesema maonesho hayo ni ya aina yake hasa kuona washiriki wa Zanzibar na nchi mbali mbali ambapo kuongezeka kwa ushiriki wao kuonesha kuwepo kwa maandalizi mazuri yanayosimamiwa na Wizara ya Biashara na maendeleo ya viwanda.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Maonesho hayo yanawapa fursa wananchi kupata huduma mbali mbali katika eneo moja tu ambazo ilikuwa wazifate  masafa marefu. Aidha Mhe. Hemed amewataka Wananchi kujitokeza na kutembelea Taasisi za Serikali zinazotoa huduma pamoja na kupata maelekezo kuhusiana na huduma wanazozitoa.

Aidha Mhe. Hemed amefurahishwa kuwepo kwa kituo jumuishi (One Stop Center) katika Maonesho hayo ambacho kinajumuisha Taasisi mbali mbali zilizoshiriki na kueleza kuwa uwepo wa Kituo hicho kunaonesha ushirikiano uliopo baina ya Taasisi mbali mbali.

Nae waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaban amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kutembelea maonesho hayo jambo ambalo linawatia hamasa Wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea maonesho hayo.

Aidha Mhe. Shaban amemuhakikishia Mhe. Hemed kuwa Wizara itaendelea kuchukua maelekezo watakayopatiwa na Viongozi mbali mbali wanaokuja kutembelea kwa lengo la kuboresha maeonesho hayo.

Akitembelea maonesho hayo Mhe. Hemed amezishauri Taasisi zinazotoa huduma kwa wananchi  kuboresha huduma zao hasa kutumia muda mfupi kuwapatia huduma wanazostahiki.