OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Ujenzi wa barabara za mjini waanza
HabariHabari Mpya

Ujenzi wa barabara za mjini waanza

Kazi ya ujenzi wa barabara mpya  za mjini ikiwa imeanza katika barabara ya Nyerere eneo la Mnazi mmoja.

Zaidi ya kilomita mia moja ya barabara pamoja na barabara za juu (flyover),  zitajengwa katika mradi huo mkubwa unaokwenda kubadilisha mandhari ya  mji.

Mradi huo unatekelezwa na Kampuni ya CCECC kutoka China.

Kuanza kwa ujenzi wa mradi huu kunafuatia ahadi aliyoitoa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kuzijenga barabara zote kuu za Mjini, Mkoa Mjini Magharibi.