OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Fainali Tawala vs Kivunge yaahirishwa
HabariHabari Mpya

Fainali Tawala vs Kivunge yaahirishwa

Fainali ya kombe la Mapinduzi Cup kwa  timu za Wizara Mashirika na Taasisi za SMZ iliyokuwa ipigwe jana kati ya Tawala na Hospitali ya Kivunge katika uwanja wa Aman imeahirika baada ya golikipa wa Tawala Bakari Juma Moh’d kuugua muda mchache kabla ya mchezo kuanza.

Nahodha  wa timu ya Tawala Said Kombo Ali alieleza kuwa hadi wanafika  uwanjani hakukua na mchezaji yoyote aliyekuwa majeruhi au kusumbuliwa na maradhi, hata hivyo mara tu baada ya kupasha moto viungo na kurudi vyumba vya wachezaji ghafla golikipa wao alianza kuugua na kuzungumza maneno yasiyoeleweka.

Kufuatia tukio hilo wachezaji wa Tawala walipata taharuki na hivyo kushindwa kuingia uwanjani kuendelea na mchezo.

Kutokana na mkasa huo kamati inayosimamia mashindano hayo iliamua kuahirisha mchezo huo na hadi tunaondoka uwanjani hakukutolewa  taarifa  yoyote juu ya mchezo huo kupigwa siku nyengine.