OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RC aridhishwa na maandalizi ya uzinduzi wa mchezo wa ngumi.
HabariHabari Mpya

RC aridhishwa na maandalizi ya uzinduzi wa mchezo wa ngumi.

Mabondia wa ngumi za kulipwa  Karim Mandonga , Dula Mbabe na Ibrahim Class wanatarajiwa kuwasili Zanzibar kesho mchana katika Bandari ya Malindi kwa  ajili ya kupima uzito kwa maandalizi ya  uzinduzi wa mchezo wa ngumi hapa Zanzibar.

Hayo yamefahamika wakati Meneja  masoko wa Kampuni  ya Tosh sport Bi Amitin Mbamba akiambata na uongozi wa kamisheni ya ngumi za kulipwa Zanzibar na Idara ya michezo walipofika Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa MjinI Magharib kuelezea kuhusu uzinduzi wa mchezo huo  .

Amefahamisha kuwa mara mabondia hao watakapowasili  watazunguka katika viunga vya maeneo mbalimbali ya Zanzibar na siku ya Jumamosi kutakuwa na tukio la kupimwa uzito kwa mabondia  hao litakalofanyika katika viwanja vya mnara wa Mapinduzi Square Michenzani.

Amewataka wananchi  wa Mkoa wa  Mjini Magharibi hususani vijana na wanamichezo kujitokeza kwa wingi katika mapokezi wa mabondia hao pamoja na tukio la kupimwa uzito

Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa ameipongeza Kamisheni ya ngumi  za Kulipwa Zanzibar  pamoja na Tosh sport  kwa  kuandaa vyema  uzinduzi wa mchezo huo na kuahidi kuwa Mkoa utatoa mashirikiano yake ili kuhakikisha mashindano hayo yanafanikiwa.

Aidha ameeleza kufarajika kwake tukokana na uzinduzi huo kufanyika ndani ya Mkoa Mjini Magharibi na kusema kuwa wameujengea heshima Mkoa huo.

Uzinduzi  rasmi wa mchezo wa ngumi hapa Zanzibar utafanyika siku ya jumapili ya tarehe 27 mwezi huu katika viwanja vya Mao ze Dong.