OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Mkoa waimarisha ulinzi Sikukuu ya Eid El Fitri
HabariHabari Mpya

Mkoa waimarisha ulinzi Sikukuu ya Eid El Fitri

Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi imesema kwamba itahakikisha hali ya ulinzi na usalama inaimarika katika maeneo mbali mbali  ili wananchi  wake waweze kusherehekea sikukuu ya Eid El fitri kwa amani na utulivu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu Sikukuu hiyo.

Amesema kuwa tayari Mkoa kupitia Kamati yake ya Ulinzi na Usalama imeshajipanga juu ya suala zima la kuimarisha ulinzi katika kipindi chote cha sikukuu yakiwemo maeneo ya yenye mikusanyiko mikubwa ya watu na  usalama wa  barabarani.

Vilevile Mkuu wa Mkoa  ameyataka Mabaraza ya Manispaa huhakikisha suala zima usafi linazingatiwa katika viwanja vya sikukuu hasa biashara ya vyakula na kuagiza viwanja vilivyoruhusiwa tu ndivyo vitumike katika sikukuu hiyo.

Amesema Viwanja vyote  vya Sikukuu vinatakiwa vifungwa saa 4:00 usiku na kumbi za muziki saa 6:00 usiku na kuvitaka vyombo vinavyohusika kulisimamia agizo hilo.

Wakati huo huo Idrissa amewataka wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao wanapokwenda katika viwanja vya sikukuu na kutowaachia kuongozana na watoto wenzao. Aidha Mkuu wa Mkoa amewatakia waislamu na wananchi wote wa Mkoa mjini Magharibi Sikukuu njema ya Eid El Fitri.