OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>PBZ yakabidhi sare kwa waendesha bodaboda
HabariHabari Mpya

PBZ yakabidhi sare kwa waendesha bodaboda

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idirisa Kitwana Mustafa ameishukuru Benki ya Watu wa Zanzibar kwa msaada wa sare kwa ajili ya waendesha Bodaboda wa Mkoa huo.

Ametoa shukurani hizo katika uwanja ya Mau ze dong wakati akikabidhi sare hizo kwa waendesha Bodaboda zilizo tolewa na benk ya watu ya Zanzibar

Amesema uvaaji wa sare hizo utasaidia kuwatambua waendesha Bodaboda na sehemu zao wanazo fanyia kazi

Aidha amesema sare hizo zitasaidia kupunguza uhalifu unaojitokeza kwa baadhi ya waendesha Bodaboda wasio waaminifu

Mkurugenzi mtendaji wa PBZ Muhsin Salim Masoud ameushukuru Mkoa kwa mashirikiano na PBZ katika kufanikisha mambo mbalimbali

Nae Katibu wa Jumuia wa Bodaboda Ali Salum Kibanga ameshukuru Serikali kwa kurasimisha Bodaboda kua ni usafiri rasmi wa kubeba abiria

Akizungumza kwa upande wa waendesha Bodaboda Mustafa Makame Mgeto amepongeza PBZ na kuahidi kuzitunza sare hizo ili waweze kutumia kwa muda mrefu