OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RC azitaka Wizara kuushirikisha Mkoa katika ujenzi wa miradi
HabariHabari Mpya

RC azitaka Wizara kuushirikisha Mkoa katika ujenzi wa miradi

Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi umezitaka Wizara mbali mbali kuushirikisha kikamilifu Mkoa huo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na uongozi wa Mkoa huo katika kikao chake  na watendaji wa Wizara ya Maji Nishati na Madini na Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ZURA kwa lengo lengo la kutatua changamoto za miundo mbinu ya maji na umeme zilizojitokeza katika ujenzi wa barabara unaoendelea maeneo mbali mbali ya Mkoa Mjini Magharibi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amesema kama Mkoa ndio wenye wajibu kisheria wa kuratibu na kusimamia  miradi yote ya maendeleo kwenye Mkoa wake, sekta husika zinapaswa kuushirikisha vilivyo Mkoa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Amesisitiza kuwa iwapo sekta hizo zitakaa pamoja na  Mkoa tangu hatua za awali za utekelezaji wa miradi, itaweza kusaidia kupunguza changamoto na malalamiko ya wananchi yanayojitokeza wakati miundo mbinu hiyo ikijengwa.

Aidha Mkoa imezitaka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), kuchukua juhudi za haraka kurudisha huduma  kwa wananchi katika maeneo ambayo yameathirika  na ujenzi wa barabara.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maji Nishati na Madini Joseph Kilangi amesema  kuna haja ya kuimarisha mashirikiano baina ya Wizara zote husika pamoja  na Mkoa  ili changamoto kama hizo zisijitokeze tena kwenye maeneo mengine ya ujenzi wa  barabara.

Nayo Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) na Shirika la Umeme (ZECO) wameshauri katika ujenzi wa barabara mbali mbali za Mkoa Mjini Magharibi kuachwa eneo la kutosha la hifadhi  ya barabara kwa ajili ya kupitisha  miundo mbinu yao ya maji na umeme. Jumla ya Kilomita 90.9 za barabara za lami zitajengwa ndani ya Mkoa Mjini Magharibi katika mradi huo