OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Zitumieni fursa zitokanazo na Kiswahili: Mhe. Majaliwa
HabariHabari Mpya

Zitumieni fursa zitokanazo na Kiswahili: Mhe. Majaliwa

Waziri Mkuu wa  Serikali ya Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  Majaliwa amewataka watanzania kuisoma lugha ya Kiswahili ili kunufaika na fursa mbali mbali zitokanazo na lugha hiyo.

Amesema licha ya kuwa lugha ya Kiswahili chimbuko lake ni Tanzania hata hiyo bado Watanzania  hawajanufaika ipasavyo na fursa  zilizopo ulimwenguni ukilinganisha na  mataifa mengine ambayo hayazungumzi kiswahili kama ilivyo hapa nchini. 

Wito huo ameutoa alipokuwa akifungua Maadhimisho ya Siku ya  Kiswahili Duniani hapo ukumbi wa Chuo  cha Polisi Ziwani.

Akizungumzia juu ya kuikuza lugha hiyo, Mheshimiwa Majaliwa  ameziagiza Wizara zenye dhamana ya kusimamia lugha ya Kiswahili  kuweka mikakati iliyo wazi katika kukikuza kiswahili sambamba na  kutoa motisha kwa wanafunzi watakaofaulu vizuri kama ilivyo kwa masomo ya sayansi. 

Sambamba na hilo  amelitaka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA), kuhakikisha lugha ya kiswahili inakuwa na kuwanufaisha Watanzania kwa kupata nafasi za kwenda kufundisha katika vyuo mbali mbali ulimwenguni.

Aidha amepongeza mijadala na makongamano yaliyofanyika takika kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani ambayo amesema yataamsha ari kwa wataalamu na wazungumzaji wa Kiswahili kuiendeleza  lugha hiyo.

Aidha Waziri Mkuu amewataka watanzania waone faghari kuzungumza kiswahili kutokana heshima iliyopewa lugha hiyo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO),  kwa kuadhimishwa kimataifa  ifikapo tarehe 7 Julai ya kila mwaka.

Katika hafla hiyo wanafunzi waliyoshinda nafasi ya kwanza katika uandishi wa Insha kutoka Tanzania Bara na kutoka Zanzibar walizawadiwa zawadi mbali mbali na fedha taslim shilingi laki tano kila mmoja.