OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RC Kitwana azifuga Baa ya Chamswa na New What app
HabariHabari Mpya

RC Kitwana azifuga Baa ya Chamswa na New What app

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Mkoa huo Mheshimiwa Idrissa Kitwana Mustafa amezifunga Baa mbili zilizopo Chukwani kufuatia vitendo viovu vinavyofanyika na kusababisha mporomoko wa maadili katika jamii hiyo.

Mkuu wa Mkoa amechukua uwamuzi huo baada ya kusikiliza malamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi  katika mkutamo maalum wa kusikiliza Kero zinazowakabili wananchi wa shehia ya Chukwani.

Amesema  kwa kipindi kirefu amekua akipokea malalamiko ya kuwepo kwa vitendo viovu ikiwemo Mpigaji wa Muziki usio na mipaka,  matendo mbalimbali ya kinyume na maadili na  hali ya  udhalilishaji wa Wanawake na Watoto jambo ambalo linaondo heshina na kuharibu maadili ya wananchi wa maeneo hayo.

Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa fursa kwa  kila mwananchi kuendesha shughuli zake za kujipatia riziki katika hali ya Amani na Utumilivu bila ya kuleta madhara kwa mtu mwengine lakini matendo yanayofanyika katika Baa ya Chamswa na Baa ya New What app  yameonesha  kukiuka Mila, utamaduni pamoja na taratibu za kisheria zilizopo katika kuendesha biashara hiyo.

Akizungumzia kuhusu suala la Amani na Utulivu ndani ya Mkoa wake Mheshimiwa Idrissa amesema kuwa hakuna mtu atakaejaribu kuvunja Amani kwa kisingizio chochote huku akitahadharisha kuwa Kamati ya Ulizi na Usalama ya Mkoa huo ipo imara wakati wowote na katika mazingira yoyote.

Kwa upande mwengine Mheshimiwa Idrissa amekemea Vitendo vinavyofanywa na baadhi ya Waumini wa Dini mbalimbali  kufanya ibada zao bila ya kujali Utamaduni na Heshima kwa wakaazi wa eneo husika.

Amesema kila Mtu ana Haki na Uhuru wa kuabudi kwa mujibu wa Imani yake hivyo sio vyema ibada ya Muumini wa Dini moja kuleta usumbufu kwa watu wengine. Hivyo amewataka wale wote ambao wanaendesha ibada zao kwa kupiga mziki kwa kiwango kisicho staki kuacha mara moja tabia hizo na kushauri kujenga kumbi maalumu kwa ajili ya kuzuia sauti ya miziki hiyo kuleta kero kwa watu wengine “ Ibada yako isilete athari kwa  mwengine kama unataka kupiga mziki wa sauti ya juu basi tengeza ukumbi wa Sound proof” alisema.

Mapema wakielelezea changamoto mbalimbali zinanazowakabi katika maeneo yao wananchi wa shehia hiyo wamesema uwepo wa Baa hizo umechangia kuharibi Mila, silka na Utamaduni za maeneo yao.

Wamesema tangu kuwepo kwa Baa hizo jamii imeathirika na mambo mbalimbali ikiwemo kukosa uhuru wa kutembea baadhi ya maeneo, Vijana na Watoto katika maeneo hayo wanaonekana kubadilika tabia huku Wazazi na walezi wakitumia muda mrefu kuwachunga watoto wao.

Aidha wananchi hao wameupongeza uwamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Kuzifungia Baa Hizo kwani kuwepo kwa Baa hizo ni kichocheo kikuu cha Uhalifu na mporomoko wa maadili kwa jamii ya maeneo hayo.

Katika hatua nyengine wananchi hao wamepongeza juhudi zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa juhudi zake za  kujenga Miundo mbinu mbalimbali ikiwemo Barabara, skuli za ghorofa na miradi mengine kwa dhamira ya kuleta maendeleo nchini.

Kadhalika wananchi hao wamesema wameridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi, kuijamii na Kisiasa.