OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Wawekezaji wakaribishwa Mkoa Mjini Magharibi
HabariHabari Mpya

Wawekezaji wakaribishwa Mkoa Mjini Magharibi

Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi imesema kwamba milango iko wazi kwa wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza katika Mkoa huo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa alipokuwa na mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa The Conferena of Black Mayors  kutoka Marekani Bi Vanesa Williams-Nash alipofika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Vuga.

Amesema katika Mkoa wake kuna fursa mbali mbali ambazo wawekezaji wanaweza  kuwekeza ikiwemo uchumi wa buluu, utalii, afya, michezo, kilimo na sekta nyenginezo.

Amemueleza Mtendaji huyo kuwa Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Dkt. Hussein Mwinyi inawakaribisha wawekezaji wenye nia njema kuja kuwekeza Zanzibar na kuiomba taasisi yake kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Zanzibar katika mataifa mengine.

Naye Bi. Vanessa amesema kuwa taasisi yake inaazma ya kufanya mkutano mkubwa wa wawekezaji hapa Zanzibar ili kushawishi  Wamarekani wenye asili ya Afika kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa Taasisi yake ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuona suala hilo linafanikiwa.