OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>MIradi ya Elimu yanufaisha Mkoa Mjini Magharibi – RC Kitwana
HabariHabari Mpya

MIradi ya Elimu yanufaisha Mkoa Mjini Magharibi – RC Kitwana

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Idrissa Kitwana Mustafa imeipongeza Benki ya Dunia kwa mashirikiano makubwa na Misaada mbali mbali ya miradi ya maendele inayoipatia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika nyanja za elimu.
Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo katika sherehe ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya lazima Zanzibar sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Skuli ya Salim Turky iliopo Mpendae.

Amesema Mkoa wa Mjini Magharibi ni mnufaika mkuu wa mradi huo pamoja na miradi mbalimbali ya elimu kwa kujengwa Skuli za Horofa na kwamba kumalizika kwa mradi huo kutaondo changamoto mbali mbali za elimu kwa wananchi wa mkoa wake na Zanzibar kwa ujumla.

Akizungumzia suala la ukuwaji wa elimu ndani ya Mkoa wake Kitwana amesema kuwa kiwango cha ukuwaji wa elimu na ufaulu kwa wanafunzi umeongezeka ukilinganicha na miaka ya nyuma. Aidha amewapongeza walimu na wanafunzi kwa kuuwasilisha vyema mkoa wa mjini Maghari katika mashindano mbali mbali katika sherehe za Elimu bila ya Malipo zilizofanyika kisiwani Pemba kwa kupata ushindi katika michezo mbalimbali.

Mapema akizindua mradi huo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kusimamia vyema mradi huo ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Amesema kiasi cha fedha Dola za kimarekani zipatazo Milioni Hamsini zitatumika katika utekelzaji wa mradi huo kwa kipindi cha miaka mitano ikiwa lengo ni kuhakikisha kuwa dhamira ya serikali kuhusu suala zima la elimu linafikiwa.

Amesema Benki ya Dunia imeamua kutoa fedha hizo ili kutimiza malengo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika suala la elimu na kwamba endapo mradi huo utekekelezwa kwa muda wa miaka Mitatu baadala ya mitano Benki ya Dunia ipo tayari kutoa Kiasi cha Dola Bilioni moja za Kimarekani.

HIvyo ni wajibu wa kila mtendaji kuhakikisha kuwa anawajibika ipasavyo katika hatua za utekelezaji wa mradi huo na endapo ikitokea msimamizi yeyote wa kushindwa kutekeleza majukumu yake katika kufanikisha mradi huo ni wajibu kuchukuliwa hatua stahiki kwa manufaa ya taifa.