OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RC ahimiza ufungaji vifaa hospitali ya Mkoa na Wilaya
HabariHabari Mpya

RC ahimiza ufungaji vifaa hospitali ya Mkoa na Wilaya

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa ameitaka Saifee Hospital Tanzania inayosimamia ufungaji wa vifaa  katika Hospitali ya Mkoa Lumumba na Hospitali za Wilaya  kukamilisha kazi hiyo kabla ya mwisho wa mwezi wa huu.

Ametoa agizo hilo akiwa katika ziara yake akiambatana pamoja na viongozi na watendaji wa Mkoa, Wilaya, Jiji na Chama cha Mapinduzi katika hospitali ya Mkoa Lumumba, hospitali ya Wilaya ya Mjini Chumbuni na Wilaya ya  Magharibi ‘B’ Mwanakwerekwe Jitimai.

Amesema pamoja na kazi kubwa iliyofanyika ya ufungaji wa vifaa hivyo, hata hivyo kuna haja ya kuongeza kasi ili kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kwa muda uliyopangwa kwa mujibu wa mkataba waliyokubaliana na Wizara ya Afya.

Mkuu wa Mkoa amewataka pia kukamilisha mifumo ya Tehama katika Hospitali hizo ili uweze kutumika kwa huduma mbali mbali za matibabu pamoja wagonjwa watakaotumia kadi za Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF), utakaoanza kutumika mwezi Oktoba 2023.

Aidha Idrissa ameipongeza Wizara ya Afya kwa hatua iliyokwisha fikiwa hadi sasa ya ufungaji wa  vifaa na utoaji wa huduma za matibabu katika hospitali ya Chumbuni na  Jitimai na kuwataka madaktari kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa watakaofika kutibiwa kwenye hospitali hizo.

Kwa upande wao Wakuu wa Wilaya hizo wamemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa maendeleo hayo makubwa yaliyopatikana ndani ya Wilaya zao kwa upande wa  sekta ta Afya.

Naye Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Msafiri Marijani amesema kukamilika kwa hospitali hiyo  ya Mkoa na hospitali za Wilaya Unguja na Pemba kunakwenda kuimarisha utoaji wa huduma za afya nchini.

Ziara hizo za Mkuu wa Mkoa zinatarajiwa kuendelea katika mirad i mbali mbali ya maendeleo ianyoendelea kujengwa katika Mkoa huo pamoja na kukutana na wananchi kusikiliza kero ziliyopo kwenye Shehia.