OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Kampeni ya msaada wa kisheria ngazi ya Mkoa yazinduliwa.
HabariHabari Mpya

Kampeni ya msaada wa kisheria ngazi ya Mkoa yazinduliwa.

Imeelezwa  kuwa uwepo wa  wasaidizi  wa sheria kunasaidia kuondoa changambato zinazowakabili wananchi katika kudai haki zao  ndani ya jamii.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa alipokuwa akitoa salamu za wananchi wa mkoa wake katika uzinduzi wa Kampeni ya  Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ngazi ya Mkoa uliofanyika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, Kikwajuni. 

Amesema kwa kipindi kirefu wasadizi hao wa sheria (Paralegal) wamekuwa wakisaidia jamii katika masuala mbali mbali ikiwemo migogoro ya ardhi, kesi za udhalilishaji na mambo mengineyo, hivyo  kampeni hiyo itakwenda kutoa msaada mkubwa zaidi wa kisheria kwa wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi.

Mkuu wa Mkoa amewataka pia wananchi wa Mkoa wake kuwa tayari kupata msaada wa kisheria kupitia kampeni hiyo wakati itakapoanza utekelezaji wake ndani ya Shehia  ili waweze kupata haki zao .

Aidha amepongeza ujio wa kampeni hiyo ambayo itatoa msaada wa kisheria kwa wananchi kwenye Shehia zote za Mkoa huo.

Makamo wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdallah ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha wananchi wasio na uwezo wanapata msaada wa kisheria pale wanapokabiliwa na masuala yanayohitaji wataalamu hao.

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar zitahakikisha kila mwananchi anapata haki yake kama sheria za nchi na maazimio ya kimaaifa yanavyoelekeza.

Kampeni hiyo ya miaka mitatu itafanyika katika mikoa yote ya Zanzibar ambapo kwa Mkoa wa Mjini Magharibi itaaza tarehe 12 Juni, 2023 katika shehia zote 121 za Mkoa huo.