OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi wamshukuru Rais Mwinyi
HabariHabari Mpya

Wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi wamshukuru Rais Mwinyi

Wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi wamemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuelekeza kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Skuli ndani ya Mkoa huo.

Shukurani hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa alipokuwa akitoa salamu za wananchi wa Mkoa huo katika uzinduzi wa Skuli ya msingi ya Salum Turky iliyopo Kwa Bintiamrani.

Amesema mafanikio yaliyopatikana katika ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta mbali mbali yametokana na maono, hekima na busara zake katika kuiongoza Zanzibar.

Katika salamu hizo pia Mkuu wa Mkoa amesema kuwa mashirikiano makubwa yaliopo baina ya Serikali na Chama cha Mapinduzi yamepelekea kufanikisha utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kiasi kikubwa.

Mkuu wa Mkoa amesema  ujenzi wa Skuli hiyo na nyengine zilizojengwa katika Mkoa wake zinakwenda kuondosha   changamoto ya msongamano wa wanafunzi katika madarasa.

Amewataka walimu waliokabidhiwa Skuli hiyo kuhakikisha wanaitunza ili iweze kubaki katika hali nzuri na kudumu kwa miaka mingi ijayo.

Akizungumza na wananchi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewapongeza viongozi wa Mkoa Mjini Magharibi na Wilaya zake kwa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye Mkoa huo.