OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>“Wafanyakazi uongezeni bidii mwaka 2023” RC Kitwana
HabariHabari Mpya

“Wafanyakazi uongezeni bidii mwaka 2023” RC Kitwana

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amewahimiza wafanyakazi wa Mkoa huo kuongeza bidii ya kazi mwaka 2023 ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.

Amesema hayo katika hafla ya wafanyakazi wa Mkoa huo kuuwaga mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka 2023 iliyofanyika Afisi ya Mkuu wa Mkoa iliopo Vuga.

Amesema katika mwaka 2022 Serikali ya awamu ya nane imefanikiwa kujenga miradi mikubwa ya maendeleo ndani ya Mkoa huo, hivyo kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake ili mipango iliyokusudiwa kutekelezwa mwaka ujao iweze kufikiwa.

Aidha Mkuu wa Mkoa amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa utekelezaji wake wa ilani ya CCM ndani ya Mkoa huo ambapo ndani ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake miradi mikubwa ya maendeleo imejengwa.

Nae Waziri wa Nchi (AR)  Katiba Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman ameupongeza Mkoa huo kwa kufanya tathmini ya utendaji wa kazi zao kwa mwaka 2022.

Amesema kitendo hicho kitaweza kuonesha kasoro zilizopo na kutafuta njia ya namna ya kuzitatua ili kuongeza ufanisi wa kazi zao.

Hafla hiyo  ilihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa na ldara Maalum za SMZ Masoud Ali Mohamed, Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa CCM  Mkoa Mjini na  Mkoa Magharibi kichama, Makatibu tawala na watendaji mbali mbali wa Mkoa na Wilaya.

Jumla ya wastaafu watatu waliofanya kazi Afisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi walitunukiwa vyeti na zawadi  katika hafla hiyo.